Habari
RAIS AL-SISI ASHINDA UCHAGUZI WA RAIS 2024
Rais wa Misri, Abdel Fattah Al-Sisi, ametangazwa rasmi na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Misri kuwa mshindi wa uchaguzi wa Rais 2024 uliofanyika tarehe 10 hadi 12 ya mwezi huu wa Disemba.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Misri imesema kuwa Al-Sisi ameshinda kwa asilimia 89.6 ya kura.
Baraza la Bunge la Misri, baraza la mawaziri na maafisa mbalimbali nchini Misri wamempongeza kutokana na ushindi huo mkubwa, wakimtakia mafanikio mema katika kuliongoza taifa la Misri.
Rais Abdel Fattah Al-Sisi anatarajiwa kuliongoza taifa la Misri hadi mwaka 2030.