ZANZIBAR NI NCHI YA KWANZA MPANGO WA WAHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII DUNIANI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema uzinduzi wa Mpango wa Kitaifa wa Wahudumu wa Afya ya Jamii Zanzibar inakuwa nchi ya kwanza Duniani kuanzisha mpango wa Kitaifa wa Wahudumu wa Afya ngazi hiyo wanaotumia mfumo wa kidijitali.
Rais Dk.Mwinyi amesema hayo katika uzinduzi wa Mpango wa Kitaifa wa Wahudumu wa Afya ya Jamii Zanzibar viwanja vya Maisara Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe:16 Desemba 2023.
Aidha Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa Serikali inathamini mchango wa wahisani katika Mpango wa Kitaifa wa Wahudumu wa Afya ya Jamii kwa jitihada zinazofanywa na Serikali kuimarisha huduma za Afya nchini .
Kwa upande mwingine amesema Serikali itaendelea kuchukua hatua za kuimarisha sekta ya afya kwa kuimarisha miundombinu na kuwepo vifaa vya kisasa vya utoaji wa huduma kwa wananchi kuhakikisha zinafika kuanzia katika ngazi ya jamii kwenye msingi hadi ngazi ya rufaa.