Habari Tofauti

MAOFISA TARAFA NA WATENDAJI KATA SHINYANGA WANOLEWA

 

 

MAOFISA  Tarafa na Watendaji wa  Kata  mkoani Shinyanga wamepatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo huku wakitakiwa kuzingatia watakayofundishwa ili kuleta ufanisi kwenye utekelezaji wa majukumu yao.

Akifunga mafunzo hayo  kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa huo,  Ofisa Elimu Mkoa, Dafroza Ndalichako, ametoa wito kwa Maofisa hao kuhakikisha wanayachukua na  kuyazingatia yale yote wanayofundishwa kwa kuwa yatawaongezea maarifa na ujuzi katika  utekelezaji wa majukumu yao.

Amesema mafunzo hayo ni muhimu katika kuisaidiasSerikali kutoa huduma bora kwa wananchi wake.

Naye, Mkurugenzi wa Idara ya   Serikali za Mitaa, Ofisi ya Rais -TAMISEMI  Hamisi Mkunga amesema Ofisi hiyo  itaendelea  kuhakikisha watumishi hao wanajengewa uwezo na kupewa mafunzo kwa ajili ya kuwa waadilifu, waaminifu na  wabunifu katika maeneo yao ya kazi

Back to top button