Habari

RAIS DK.MWINYI AFUNGUA FURSA ZA UCHUMI KWA WAROMANIA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema ukuaji wa Zanzibar na ustawi wa siku zijazo unategemea uwekezaji, biashara, uchumi wa buluu na utalii.

Rais Dk.Mwinyi amemkaribisha Zanzibar Rais wa Romania Mhe.Klaus Lohannis na kampuni za nchini hiyo kufanya kazi pamoja katika masuala ya biashara, uwekezaji, uchumi wa buluu, utalii na sekta nyinginezo zenye maslahi kwa maendeleo.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo wakati hafla ya chakula cha mchana aliyomwandalia  mgeni wake huyo Ikulu Zanzibar tarehe 18 Novemba 2023.

Kwa upande wake Rais huyo wa Romania  amesema  Romania itaendeleza ushirikiano ikiwemo kujumuisha  kampuni za Romania  kwa kuanzisha biashara mpya Zanzibar, kukuza utalii, uchumi wa buluu, uwekezaji, pamoja na mabadilishano ya utamaduni na usimamizi wa urithi .

Back to top button