Habari Tofauti

DK.MWINYI AWATAKA WAJASIRIAMALI WACHANGAMKIE FURSA ZA MIKOPO BILA YA RIBA

0:00

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema mpaka kufikia mwaka 2025 atakuwa ameshatimiza ahadi  zote alizozitoa wakati wa kampeni ikiwemo maeneo mazuri ya kufanya biashara, mitaji pamoja na kodi nafuu katika masoko wanapofanyia biashara zao.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo wakati  alipofungua jengo la wajasiriamali Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba leo tarehe 02 Novemba 2023.

Vilevile ameleeza kuwa  shilingi bilioni 31  zilizowekwa na Serikali katika benki ya CRDB wajasiriamali wameendelea kukopa bila ya riba kwa sababu riba zote zinabebwa na Serikali.

Aidha Rais Dk.Mwinyi amewahimiza wajasiriamali waliokuwa kwenye maeneo rasmi waendelee kuomba mitaji hiyo ya Serikali ambayo haina riba.

Pia ametoa miezi mitatu bure bila kulipa kodi kwa wajasiriamali wa kituo cha Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba

Back to top button