Habari Tofauti

Dkt. Sweilam akutana na Naibu Waziri wa Maji na maji takataka wa Jamhuri ya Afrika Kusini

0:00

Kabla ya uzinduzi wa shughuli za “Wiki ya Maji ya Sita ya Kairo” kwa ufadhili wa Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri… Dkt. Hany Sweiam akiteta jambo na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.David Malupo, Naibu Waziri wa Maji na Usafi wa Mazingira wa Afrika Kusini.

Dkt. Swailem amesema kuwa Wiki ya Maji ya Kairo inawaleta pamoja wataalamu wengi katika uwanja wa maji kutoka nchi zote Duniani, akielezea furaha yake kwa ushiriki wa Afrika Kusini katika Wiki ya Kairo. Dkt. Sweilam alisisitiza mahusiano ya kipekee kati ya Misri na Afrika Kusini katika ngazi zote, akielezea nia ya Misri kusaidia ushirikiano na nchi mbalimbali za Afrika.

Dkt. Swailem ameualika upande wa Afrika Kusini kushiriki katika Mpango wa Kimataifa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi katika Sekta ya Maji (AWARe), unaolenga kutekeleza miradi ya kukabiliana na mabadiliko katika sekta ya maji katika nchi za Afrika, na kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa sekta ya maji kutoka nchi za Afrika kupitia “Kituo cha Afrika cha Mafunzo na Kujenga Uwezo katika uwanja wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi”, kilichoanzishwa ukiambatanishwa na mpango huo, akiashiria kuongezeka kwa mahitaji ya nchi za Afrika kushiriki katika mpango huo muhimu.

Dkt. Swailem alisisitiza kuwa hatua muhimu kwa sasa zinachukuliwa ili kutia saini mkataba wa maelewano katika nyanja ya usimamizi wa rasilimali za maji kati ya nchi hizo mbili. Kwa upande wake, Naibu Waziri huyo wa Afrika Kusini alieleza kufurahishwa kwake na mkutano huo unaothibitisha nguvu ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili, akisisitiza nia ya nchi yake ya kuimarisha ushirikiano na Misri haswa katika uwanja wa rasilimali za maji.

Back to top button