Habari

RAIS DK.MWINYI AVIPONGEZA VIKOSI VYA SMZ

 Kamanda Mkuu wa Idara Maalum ya Vikosi vya  SMZ, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amevipongeza vikosi vya SMZ kwa kazi kubwa wanazozifanya kwa kuhakikisha amani na utulivu wa nchi, kushiriki kazi za uzalishaji mali , ujenzi wa miradi mbalimbali, kujenga uwezo na ujuzi kwa vijana , uanzishwaji wa viwanda, malezi kwa vijana na kuwafanya wawe wazalendo kwa mafunzo yanayotolewa, kutoa huduma kwa jamii ikiwemo elimu, tiba akitolea mfano wa hospitali ya KMKM.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo leo tarehe 30 Oktoba 2023 alipozungumza  na Maafisa pamoja na Wapiganaji wa Idara Maalum za SMZ  katika  uwanja wa JKU-Kama Mkoa wa Mjini Magharibi.

Idara Maalum ya Vikosi vya SMZ inaundwa na JKU, KMKM, KVZ, Zimamoto na Uokozi pamoja na Chuo cha Mafunzo.

Back to top button