Habari Tofauti

MAGARI HAYA MSIYAPELEKE KIMYA KIMYA KWENYE MIKOA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amewataka Wakuu wa Mikoa yote Tanzania bara kutopeleka magari ya kubebea wagonjwa waliyokabidhiwa leo kimya kimya bali wajulishe viongozi wa chama Tawala pamoja na wananchi kuwa sasa huduma za usafiri kwa wagonjwa yameongezeka tofauto na hapo awali.

Waziri Mchengerwa ameyasema hayo leo wakati akizungumza kwenye Uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria Tanzania ya mwaka 2022 na Ugawaji wa Magari ya Kubebea Wagonjwa na vifaa tiba uliofanyika kwenye ukumbi wa kumataifa wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es salaam leo tarehe 28.10.2023.

Ripoti hiyo inazinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Back to top button