Habari

ZANZIBAR MWENYEJI MKUTANO WA 20 WA BENKI YA DUNIA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania Nathan Balete na ujumbe wake Ikulu Zanzibar leo tarehe 27 Oktoba 2023

Katika mazungumzo yao wamegusia ushirikiano uliopo kati ya Benki ya Dunia na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo uchumi wa buluu , sekta ya nishati hususani  umeme wa jua, upepo na suala la gesi asilia, elimu, afya, kilimo, kujenga uwezo na msaada wa kiufundi, uwezeshaji wa Wanawake, Mahakama na mengineyo.

Aidha Rais Dk.Mwinyi ameishukuru Benki ya Dunia kwa kuendelea kuisaidia Zanzibar  katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

Naye Waziri wa  Nchi ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Dk.Saada Mkuya amesema Zanzibar  itakuwa mwenyeji wa mkutano wa 20 wa mapitio wa Benki ya Dunia utakaoshirikisha wajumbe 350 kutoka nchi mbalimbali duniani.

Mkutano huo pia utahudhuriwa na Rais wa Benki ya Dunia Ajay Banga kuanzia tarehe 06 hadi 08 Disemba mwaka huu katika Hoteli ya Golden  Tulip  Airpot  Mkoa wa Mjini Magharibi.

Back to top button