NYUMBA ZA WALIMU ZA KUTOSHA KUJENGWA MWAKA WA FEDHA 2024/25
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema fedha za ujenzi wa nyumba za walimu za kutosha zitatengwa kwenye Bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha 2024/25.
Mhe.Rais Samia ameyasema hayo leo Oktoba 16, 2023 alipokuwa akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Mkalama mara baada ya kufungua daraja la msingi lililojengwa kwenye Kata ya Msingi, mkoani Singida.
“Nimearifiwa na Mbunge wenu kuwa kuna uhitaji mkubwa wa nyumba za walimu katika Halmashauri hii habari njema ni kuwa jambo hili tutalipa kipaumbele kwenye bajeti ya mwaka 2024/25 na nyumba za walimu zitajengwa za kutosha ili walimu waweze kukaa karibu na maeneo ya shule.”
“Nimearifiwa kuna
upungufu wa walimu asilimia 40 kwa shule za msingi na asilimia 20 kwa shule za Sekondari hivyo hili tumelichukua na Waziri wa TAMISEMI yupo hapa atakwenda kulifanyia kazi,”amesema.
Aidha, ameitaka Halmashauri ya Wilaya hiyo kujipanga kujenga matundu ya vyoo kwenye shule kwa kuwa serikali kuu imepunguza kwa kiwango kikubwa upungufu wa vyumba madarasa.
Kuhusu ombi la Halmashauri kupatiwa vituo viwili vya Afya, Mhe. Rais amesema kupitia vituo vipya 214 vitakavyojengwa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI kimoja kitajengwa katika Kata ya Iguguno