TIMU YA TAMISEMI YASHINDA NAFASI YA PILI MCHEZO WA DRAFTI – SHIMIWI
Timu ya TAMISEMI wanawake mchezo wa drafti imeshinda nafasi ya pili dhidi ya mpinzani wake timu ya Mawasiliano katika Michezo ya Shirikisho ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI).
Mchezo uliochezwa Oktoba 12, 2023 katika viwanja vya chuo Kikuu cha RUAHA Mkoani Iringa.
TAMISEMI SPORTS CLUB inaendelea kufanya vizuri katika michezo ya SHIMIWI kwa mwaka 2023 kwa michezo iliyoshiriki kuwa bingwa mchezo wa vishale(DARTS) karata kufikia hatua ya robo fainali kwa upande wa wanawake na wanaume, mchezo wa kuvuta kamba kuingia hatua ya robo fainali na mchezo wa netinoli kuingia hatua ya mtoano.
Mashindano ya SHIMIWI kwa watumishi wa Wizara, Idara za Serikali yamekua na manufaa kwa watumishi hao kuweza kujifunza mengi hasa kuhusu michezo na sheria zake.