Habari Tofauti

KAMATI YA TAMISEMI YAWATAKA TANGA JIJI KUWASILISHA TAARIFA YA UJENZI WA DAMPO

 

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Denis Londo imenyooshea kidole ujenzi wa Jalala kuu la Kisasa (Dampo) lililojengwa katika kata ya Chongoleani kwenye Halmashauri ya Jiji la Tanga kupitia mradi wa Uendelezaji Miji na Majiji (TSCP).

Kamati hiyo iliyopo kwenye ziara ya kikazi mkoani humo ilitembelea Dampo hilo tarehe 12.10.2023 na kubaini hitilifu katika ujenzi na ubora wa Dampo hilo linahudumia wakazi wa Jiji lote la Tanga.

Kufuatia hali hiyo Kamati imemtaka Mkurugenzi wa Jiji la Tanga kuwasilisha taarifa halisi ya utekelezaji wa mradi huo mbele ya Kamati pamoja na andiko la mradi la mradi huo ili kujua kilichoandikwa na kukinganisha na utekelezaji wake.

Katika ziara hiyo ilianzia Mikoa na Iringa na Morogoro kukagua miradi iliyotekelezwa kupitia TSCP na ULGSP na kuangalia maandalizi ya utekelezaji wa mradi wa TACTIC Kamati imeielekeza TARURA kuangalia mfumo mzima wa uchakataji wa maombi na upelekaji wa fedha za miradi mikubwa katika baadhi ya Miji  na Tanga ikiwa moja wapo”

Pia Kamati imetoa maelekezo ya kwa Halmashauro zote ambazo zimetekeleza miradi hii kuangalia namna bora ya kusimamia mitambo, magari,mashine na vifaa vingine vyote ambavyo vipo chini ya  Halmashauri zote hizo ili vitumike kwa ufanisi na kwa muda mrefu.

Back to top button