Habari

SERIKALI KUAJIRI WAHUDUMU WA AFYA 153,000 NGAZI YA  JAMII

Ili kufikia lengo la Serikali kuhakikisha huduma za afya zinamfikia kila mtanzania, Serikali itaajiri wahudumu wa afya ngazi ya kamii  jamii 153,000  katika kipindi cha miaka mitatu.

Taarifa hiyo imetolewa leo na Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI( Afya) Dkt. Wilson Charles Mahera wakati wa kufunga kikao cha hitimisho  la mradi wa TUIMARISHE AFYA uliokuwa unaendeshwa kwa ushirikiano kati ya  Shirika la Maendeleo la Uswisi, Ofosi ya Rais TAMISEMI pamoja na Wizara ya Afya.

“ Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Dkt.Samia Suluhu Hassan ina lengo la kufikisha huduma za afya kwa kila mtanzania na ndio maana kuna uwekezaji mkubwa wa ujenzi wa  vituo vya kutolea huduma za afya na vifaa tiba vya kisasa.

Vituo hivyo vya kutolea huduma za afya vinahitaji watoa huduma  na katika miaka mitatu ijayo tutaajiri jumla ya wahudumu wa afya jamii (WAJA) 153,000 amesema.

Dkt Mahera ameongeza kuwa Serikali inaandaa mitaala ambayo itatumika kuwafundisha wahudumu hao na mpango huo wa kuajiri wahudumu hao  utagharimu jumla ya shilingi Trilioni moja na milioni mia moja (1.1 Tirioni).

“ Serikali inataka wahudumu wote wa afya ngazi ya jamii wajengewe uwezo wa kuhudumia wananchi hivyo tunakaribisha ushirikiano kutoka kwa wadau wote ili tufanikishe mpango huu kwani ukikamilika utaleta mageuzi makubwa kwenye afya ya msingi nchini” Amesema Dkt.Mahera

Back to top button