Misri yaunga mkono juhudi za Côte d’Ivoire za kuanzisha kituo maarufu cha kikanda cha upasuaji wa ini na upandikizaji wake
Rahma Ragab

Dkt. Wael Badwy, Balozi wa Jamhuri ya kiarabu ya Misri kwenye Côte d’Ivoire alikabidhi vifaa vya kitiba vinatolewa na Misri ili kuunga mkono uanzishaji wa kituo maarufu cha kikanda cha ubora wa upasuaji wa ini na upandikizaji wake kwenye hospitali ya chuo kikuu ya TREICHVILLE mjini Abidjan.
Waziri wa afya wa Ivoire, Pierre Dimba amepokea vifaa vya kitiba na hiyo kwa mahudhurio ya Dkt. Elie Keli , mwenyekiti wa sehemu ya upasuaji wa umma na mfumo wa umeng’enyaji kwenye hospitali.
Balozi wa Misri ameeleza kwamba misaada hiyo ni miongoni mwa programu ya ushirikiano wa matibabu kati ya Misri na Côte d’Ivoire, ulioshuhudia timu ya matibabu ya kimisri ilifanya upandikizaji wa kwanza wa ini Afrika Magharibi katika Hospitali ya Chuo kikuu cha TREICHVILLE huko Abidjan mwaka 2021.
Na akasisitiza kwamba Misri inaunga mkono juhudi za Côte d’Ivoire kuanzisha kituo cha kikanda cha ubora kwa upasuaji wa ini na upandikizaji, ambapo pande hizo mbili zinashirikiana kutoa mafunzo kwa madaktari na wauguzi wa Ivory Coast muhimu kuendesha kituo hicho.
Kwa upande wake, Waziri wa Afya wa Ivory Coast alieleza shukrani za Rais Alassane Ouattara na serikali ya Ivory Coast kwa Misri kwa zawadi hii, akipongeza ushirikiano na Misri, ambayo aliielezea kama mfano wa ushirikiano wa Kusini na Kusini. Alisisitiza kuwa matumizi ya vifaa hivi yataongezwa ili kutibu wagonjwa wengi iwezekanavyo.