Habari

SOKO LA KARIAKOO LIENDESHWE KWA MFUMO WA SOKO LA KIMATAIFA

Kamati ya Kudumu ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imetoa rai kwa viongozi wanaosimamia Shirika  la Masoko kariakoo kukaa na kutengeneza mfumo wa utawala na uendeshaji unaoendana na soko la kimataifa.

Akizungimza Makamu Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Julius Nyamoga walipotembelea kuona maendeleo ya ujenzi wa soko hilo mwishoni mwa wiki iliyopita amesema  tunaweza kuwa na jengo zuri, miundombinu mizuri na ya kisasa  lakini uendeshaji wa Soko hilo ukawa sio wakawaida usioakisi hadhi ya majengo yaliyopo.

Amesema Soko la Kariakoo linatakiwa kuendeshwa Kimataifa na lijibu changamoto za wafanyabiashara wa ndani na wa nje ambao wamehudumiwa katika soko hilo kwa muda mrefu.

Pia kamati amewataka Uongozi wa Shirika la  soko kuweka utaratibu mzuri na mwelekeo wa mifumo ya uchakataji taka kuanzia ukusanyaji wake mpaka kuondolewa ili kuweza kuondoa adha hiyo kwa wafanyabiashara.

“Tunatoa msisitizo kuhusu ugawaji wa vizimba na maduka na sehemu zote za biashara kwamba uwe na uwazi na uzingatie wafanyabiashara waliokuwepo kabla ya soko kuungua na kama kutakuwa na watu wengine wanahitaji basi kuwe na vigezo ambavyo vinausawa na ambavyo haviwezi kutoa fursa ya upendeleo kwa baadhi ya watu ili kusiwe na malalamiko”

Mhe.Nyamoga amemalizia kwa kutaka soko hilo likamilike kwa wakati na wakandarasi wasisitizwe kuhusu muda ambao  soko hilo linatakiwa kukamilika  ili huduma zianze kufanyika na wananchi waanza kupata huduma mapema.

Back to top button