DKT. MSONDE AUNGANA NA VIONGOZI WA NCHI ZINAZOSHIRIKI FEASSSA

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais TAMISEMI (Elimu), Dkt. Charles Msonde amekutana na kuzungumza na Waziri wa Elimu wa Rwanda, Dkt. Valentine Uwamariya pamoja na viongozi wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zinazoshiriki katika Mashindano ya michezo ya shule za Msingi na Sekondari (FEASSSA) wakiongozwa na Mwenyekiti wake, Bw. Justus Mugisha.
Mazungumzo hayo yamefanyika wakati wa Chakula cha Pamoja na viongozi wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zinazoshiriki katika Mashindano ya michezo ya shule za Msingi na Sekondari yanayofanyika katika Mji wa Huye nchini Rwanda.
Dkt. Msonde amembatana na Mkurugenzi wa Usimamizi wa Elimu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mwl. Vicent Kayombo na Wakurugenzi wasaidizi ikiwa ni pamoja na Bw.George Mbijima na Bw. Yusuph Singo.