Habari Tofauti

WAKULIMA WA MIWA KUNUFAIKA NA UPANUZI WA KIWANDA CHA SUKARI KILOMBERO

0:00

Wakulima wa zao la Miwa Wilayani Kilombero,wanatarajiwa kunufaika kiuchumi na kijamii kutokana na ongezeko la uhitaji wa Miwa katika kiwanda kipya cha Sukari Kilombero(K4).

Hayo yamesemwa leo Agosti 16 2023 katika ziara maalum iliyofanywa na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Adv.Dunstan Kyobya akiambatana na Kamati ya Ulinzi ma Usalama ya Wilaya pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara alipotembelea Kiwandani hapo kufatilia maendeleo ya upanuzi wa kiwanda hicho kinachotarajiwa kukamilila Julai 2024.

Akiweka wazi manufaa watakayopata wakulima hao,Mkuu wa Idara ya Kilimo wa Kampuni ya Sukari Kilombero Ndg.Pierre Redinger amesema kuwa kwasasa Tani 600,000 husindikwa kwa msimu wakati Kiwanda kipya kinauwezo wa kusindika Tan 1500,000 na hivyo kuwepo  na uhitaji wa Tani 900,000 za Miwa kwa msimu.

Aidha kutokana na ongezeko hilo mapato ya wakulima yataongezeka kutoka Sh.Bilioni 75 mpaka Sh.Bilioni 165 kwa msimu na kusababisha kuongezeka kwa pato la kukuza uchumi wa Nchi kutoka Sh.Bilioni 340 mpaka Sh.Bilioni 750 kwa msim.

Kwa upande wake Mchumi wa Bodi ya Sukari Tanzania Joshua Mhando,ameeleza hatua zilizochukuliwa na Bodi hiyo ili kutimiza malengo yaliyoazimiwa katika kumnufaisha mkulima mmoja mmoja ni pamoja na;

Kuwasajili wakulima wote katika mfumo maalum wa kidijitali unaomuwezesha kuuza Miwa kiwandani hapo ikiwa ni moja ya vigezo vilivyoafikiwa vya ununuzi wa Miwa sambamba na kusimmaia mikataba kupitia wanasheria wa Bodi ya Sukari na kuhakikisha kila mmoja anapata stahiki zake ipasavyo kati ya mnunuzi na muuzaji.

Hata hivyo DC kyobya amewataka wawekezaji wa Kiwanda hicho kuwatumia vizuri Wanahabari ili kujenga uelewa wa pamoja kwa wananchi juu ya Kiwanda hicho.

IKumbukwe kuwa ILOVO niwamiliki wa Kampuni ya Sukari Kilombero kwa 75% na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania niwamiliki  kwa 25%.

Back to top button