Habari

RAIS DK.MWINYI ASEMA SERA MPYA YA VIJANA KUZINDULIWA ZANZIBAR

0:00

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa matayarisho ya sera mpya ya maendeleo ya Vijana Zanzibar yamekamilika na itazinduliwa hivi karibuni na kuanza kazi rasmi.

Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 12 Agosti 2023 wakati akifunga kilele cha maadhimisho ya siku ya Vijana kimataifa, na kupokea maandamano ya Vijana kutoka Taasisi mbalimbali za Vijana kutoka Taasisi  binafsi, za Serikali, Vyama vya siasa pia ametembelea mabanda mbalimbali ya  Taasisi za vijana yaliyofanyika viwanja vya Maisara, Zanzibar  .

Rais Dk.Mwinyi ametoa wito kwa taasisi na wadau mbalimbali wa maendeleo ya Vijana na Mazingira kuendelea kuwekeza katika kuimarisha elimu na uchumi wa kijani kwa Vijana.

Vilevile, Serikali imetoa zaidi ya shilingi bilioni 16.8 kupitia wakala wa uwezeshaji wananchi kiuchumi kwa wajasiriamali wadogo wadogo hususani wanufaika ni vijana kwa sehemu kubwa.

Back to top button