Habari Tofauti

HALMASHAURI ZOTE ZATAKIWA KUANDAA MPANGO WA MAENDELEO WA KILIMO

Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Dkt. Festo J. Dugange(Mb) amezita Halmashauri zote nchini kuandaa mpango wa Maendeleo wa kilimo unaoendana na hali halisi ya wilaya huska ili kuwawezesha Wananchi Kuzalisha kwa tija katika maeneo yao.

Ameyasema hayo wakati wakati alipotembelea na kukagua mabanda katika Maneosho ya wakulima ya Kimataifa Nanenane kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

“Halmashauri ambapo bado hazijaandaa Mipango ya Maendeleo ya kilimo zihakikishe zinafanya utafiti na ubunifu kwa kuandaa mpango huo katika maeneo yao ili kuibua fursa ili kuboresha uzalishaji”

Amesema katika kipindi cha nyuma kulikuwa na Mipango   ya maendeleo iliyokuwa inayoijumuisha nchi nzima ambayo haikuwa na ufanisi kwa sababu wilaya zinatofautiana kwa misimu na hali ya hewa na shughuli za kiuchumi.

Dkt. Dugange amesema dira na maelekezo ya Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kutaka kuona wakulima, Wavuvi na wafugaji wanazalisha kwa tija katika kazi wanazojishughulisha nazo.

Aidha, Dkt. Dugange ameziagiza Halmashauri kuendelea kuwajengea uwezo wajasiriamali ili wanapopata mikopo ya asilimia 10 iweze kuwakwamua kiuchumi kwa kuwatoa hatua waliyopo kwenda hatua nyingine.

“Urejeshaji wa mikopo umekuwa chini kwa sababu ya uelewa, Wananchi ili wapate tija na kutumia fursa vizuri za Mikopo hiyo lazima wajengewe Uwezo, kwa kuelewa nini cha kufanya au wazalishe nini, kwa wakati gani na  wapi watapata Soko la uhakika”  amesisitiza Dkt. Dugange

Back to top button