Habari Tofauti
NDEJEMBI AONGOZA KIKAO CHA MAANDALIZI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA BONDE LA MTO MSIMBAZI NA DMDP 2
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali, Mhe. Deo J. Ndejembi (Mb) ameongoza kikao cha Wataalam kwa ajili ya kujadili maandalizi ya Utekelezaji wa Miradi ya Bonde la Mto Msimbazi na Mradi wa Uendelezaji Jiji la Dar es Salaam awamu ya pili (DMDP 2).
Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 03 Agosti 2023 katika Ofisi za TAMISEMI, Mtumba Dodoma na kuhudhuliwa na Watalaam kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) pamoja na Waratibu wa Mradi wa uendelezaji Jiji la Dar es Salaam (DMDP).