Habari Tofauti

RC  MALIMA  ARIDHISHWA NA UTEKELEZWAJI UJENZI WA KIWANDA CHA SUKARI KILOMBERO K4

 

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Kighoma Malima, ametembele kiwanda cha sukari Kilombero na kujionea maendeleo ya maandalizi ya ujenzi wa kiwanda kipya cha sukari K4 sambamba na kushuhudia uchakataji wa miwa hadi kuwa sukari kiwandani hapo.

Ameyafanya hayo leo Julai 22,2023 alipotembelea katika kampuni ya uzalishaji Sukari Kilombero inayopatikana wilaya ya Kilombero katika Halmashauri zake za Ifakara Mji na Kilosa.

Aidha amempongeza Meneja wa kilombero sugar company Limited Guy William kwa kuonesha ushirikiano kwa serikali katika kuchangia  mapato ya nchi kwa kulipa ushuru kupitia Halmashauri za wilaya hiyo na kutoa ajira kwa wananchi

Sanjari na hayo amewataka wakulima wa miwa kutoa ushirikiano kwa Serikali katika kutekeleza maagizo yake ili kufikia malengo ya uzalishaji kwakuwa wao ni wanufaika wa Karibu zaidi wa kiwanda hicho.

“Kutokana na nia njema ya serikali yetu inayoongozwa na Rais wetu  Mhe.Samia Suluhu Hassan,tumejipanga vyema kuhakikisha wakulima wa miwa wanaongeza uzalishaji unaoendana na uhitaji wa Kiwanda kinachojengwa kwa kuwapa elim bora ya kilimo na kuwawezesha kupata pembejeo stahiki za kilimo kwa kushirikiana na bodi ya sukari Tanzania”.amesema Malima.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa biashara kiwandani hapo Fimbo Mwitala ameipongeza serikali kwa kuendelea kuunga mkono uendeshaji wa shughuli za uzalishaji wa sukari kiwandani hapo na kuwataka wananchi kutumia sukari kutoka kilombero sugar kwakua ni yenye kukidhi mahitaji yao kutokana na bei rafiki na namna ilivyohifadhiwa kwa kuzingatia usalama wao kiafya.

Kiwanda cha Kilombero Sugar kinamilikiwa na Illovo kwa 75% na serikali ya Tanzania kwa 25% ambapo licha ya kuwa na manufaa kwa wanachi kupitia ajira na biashara lakini pia kina mchango mkubwa katika uboreshaji wa huduma za kijamii.

Back to top button