Waziri wa Mipango na Maendeleo ya Uchumi ajadili njia za ushirkiano na naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
Bassant Hazem
Dkt.Hala El-Said, Waziri wa Mipango na Maendeleo ya Uchumi, alikutana na Bi. Amina Mohammed, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, pembezoni mwa ushiriki wake katika Jukwaa la Siasa la Juu la Maendeleo Endelevu (HLPF) 2023 lililofanyika New York chini ya kauli mbiu “Kuharakisha kupona kutokana na Virusi vya Corona na utekelezaji kamili wa Ajenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu katika ngazi zote”.
Kupitia mkutano,Dkt El-Said alithibitisha ahadi ya Misri ya kufikia malengo ya maendeleo endelevu, akibainisha maendeleo yaliyofanywa na serikali katika suala hilo, na Misri kwa sasa inalenga katika kuweka malengo ya maendeleo endelevu katika ngazi ya mkoa, ambapo ripoti 27 zilizinduliwa ili kuweka malengo ya maendeleo endelevu katika majimbo kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu, na ripoti hizo zinalenga kuandika maendeleo na hali ya sasa ya kutekeleza malengo ya Maendeleo Endelevu katika kila mkoa, na ushirikiano umefanywa na Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa kusaidia majimbo 3 ya Misri – kama hatua ya kwanza – Fayoum, Beheira na Port Said ni katika kuendeleza mapitio ya kwanza ya hiari ya ndani (VLRs) ambayo husaidia serikali za mitaa kushiriki maendeleo katika kufikia SDGs kwa njia shirikishi.
Al-Said pia aligusia umuhimu wa suala la fedha kwa ajili ya maendeleo, umuhimu wa kusaidia nchi zilizoendelea na za kati katika suala hilo, na kurekebisha mfumo wa kifedha Duniani.
Waziri huyo aliongeza kuwa nchi zilizoendelea, ikiwa ni pamoja na Misri, zimeweza, licha ya changamoto za kimataifa mnamo vipindi vya hivi karibuni, kufanya maendeleo ya ajabu, akisisitiza kuwa mkutano ujao wa maendeleo endelevu lazima uweke hatua kwa nchi zilizoendelea kusaidia nchi za hali ya kati ya maendeleo na zinazoendelea.