Habari Tofauti

Mkurugenzi Idara ya Elimu Sekondari akutana na Walimu Wakuu wa Mkoa wa Kusini Unguja

Mkurugenzi Idara ya Elimu Sekondari amekutana na Walimu Wakuu wa Mkoa wa Kusini Unguja katika ukumbi wa walimu TC Dunga.

Lengo la kikao hicho ni kuhakikisha taarifa za walimu katika skuli zao zinapatikana ambapo itasaidia kuweza kujua mahitaji halisi ya walimu pamoja na miundombinu mengine ya kielimu kama maktaba, maabara,vyoo na samani.
Pia uhakiki husaidia kupata kujua taarifa za walimu wagonjwa,walioko masomoni na ambao wamepangia kazi nyepesi kutokana na ugonjwa waliokuwa nao.


Sambamba na hayo Mkurugenzi ametumia nafasi hiyo kuwasisitiza walimu wakuu kuwa makini na kusimamia kazi zao kwa uweledi na kuhakikisha wanalinda rasilimali za Serikali zilizoko katika maeneo ya skuli zao.
Kazi hiyo ya uhakiki ilifanywa kwa mashirikiano na watendaji wa idara ya Sekondari Wizara ya Elimu Zanzibar.

Back to top button