Habari Tofauti

WAZIRI JAFO AFANYA ZIARA ZBC

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo ametembelea Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC). Akiwasili kituoni hapo Mhe. Jafo amepokelewa na Mkurugenzi wa Habari na Matukio wa Bw. Salum Ramadhani Abdallah.

Dkt. Jafo alitembelea kituo hicho  siku ya Jumatatu (Julai 10, 2023) ili kuona shughuli mbalimbali zinafanywa na kituo hicho pamoja na kushiriki kipindi cha mahojiano ya moja kwa moja (LIVE) cha taarifa ya Habari cha Baraza kinachorushwa na Kituo cha Utangazaji cha Televisheni cha Shirika hilo kilichopo eneo la Mnazimmoja Zanzibar.

 

Back to top button