Timu ya kitaifa ya utekelezaji wa mradi wa kuboresha elimu ya awali na Msingi wakutana

Timu ya kitaifa ya utekelezaji wa mradi wa kuboresha elimu ya awali na Msingi (Boost ) wamekutana leo Julai 7, 2023 mkoani Morogoro katika kikao kazi cha kuandaa taarifa ya utekelezaji wa mradi kwa mwaka 2022/23 na mkakati wa utekelezaji wa mradi kwa mwaka 2023/24.
Timu hiyo inahusisha wataalamu kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Taasidi ya elimu Tanzania , Wakala wa Maendeleo na Uongozi wa Elimu( ADEM) , Baraza la Mitihani na Tume ya Utumishi wa walimu (TSG).
Akitoa salamu kwa timu hiyo Katibu wa Tume ya Utumishi wa walimu Mwl.Paulina Nkwama kuhakikisha wanajadili kwa kina mpango kazi wa mradi huo na kuhakikisha unaleta mabadiliko katika sekta ya Elimu
Amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya Sekta ya Elimu nchini hivyo amewataka wataalam kusimamia miradi ili iweze kukamilika kwa wakati