Habari Tofauti

WALIMU WA SHULE ZA AWALI WATAKIWA KUWA WABUNIFU

Angela Msimbira, KONDOA

 

 

Afiisa elimu ya awali na Msingi Halmashauri ya Mji wa Kondoa Hassan Mtamba amewataka walimu wa awali kuwa wabunifu kwa kubuni zana bora za kufundishia watoto ili wajitambue na kuwa na mwitikio chanya akiwa nyumbani na shuleni

Akifunga Mafunzo ya walimu wa awali yaliyofanyika katika Chuo cha Ualimu Bustani, Halmashauri ya Mji wa Kondoa Mkoani Dodoma amesema lengo mafinzo ni kuwajengea uwezo waalimu wa awali ili kuwawezesha ujifunzaji wa mtoto wenye tija

Amewataka walimu wa elimu ya awali kuhakikisha wanatumia ujuzi na maarifa waliyoyapata kwenye mafunzo hayo katika kubuni mbinu mahiri za ufundishaji zitakazowezesha watoto kuelewa kwa haraka na kujenga Taifa lenye ujuzi

“Tunaamini kabisa mafunzo haya yatawasaidia, inashangaza mmekaa siku 3 mkatengeneza zana,halafu mkashindwa kutimiza wajibu wenu, hii si sahihi kabisa nendeni mkatumie mafunzo haya katika ufundishaji wa watoto wetu” amesisitiza Mtamba

Amewataka kuhakikisha wanatumia zana za ufundishaji zinazopatikana katika mazingira waliopo ili

watoto waweze kupenda kujifunza stadi mbalimbali

Akiongea kwa niaba ya washiriki Mwalimu Mwanamkisi Mbaraka ameishukuru Serikali kea kuhakikisha walimu wa elimu ya awali wanapatiwa mafunzo ambayo yatasaidia kuleta mabadiliko kwenye ufundishaji wa watoto.

 

Back to top button