RAIS DK.MWINYI AHITIMISHA ZIARA YAKE CHINA AREJEA NCHINI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi amesema atawasaidia wawekezaji wanaokumbana na vikwazo na changamoto mbalimbali.
Dk. Mwinyi aliyasema hayo alipozungumza na wawekezaji wa kampuni mbalimbali za China waliofika kuzungumza naye kuhusiana na fursa za uwekezaji zinazopatikana Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.
Akizungumza na Mwenyekiti wa kundi la kampuni za Liyu Group, Bw. Yuefeng Wang wanaojishughulisha na utengenezaji viatu na kuzalisha umeme, amemwambia nishati kwa sasa inahitajika zaidi Zanzibar kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya viwandani. Muhimu ijulikane gharama zao na aina ya umeme.
Kuhusu biashara ya viatu Dk. Mwinyi aliwashauri wawekezaji hao kuangalia soko pana la Afrika.
Aidha alikutana na Bw. Quan Chen wa Kampuni iliyopo Tanzania, iitwayo Tanzania Binjiang inyoshughulika na usindikaji wa nyama na kumwarifu soko la nyama lipo kubwa. Ila afuate tu taratibu.
Pia alikutana na Bi.Xiaoli Zhou mwekezaji wa utalii wa michezo na Mh. Rais akamkaribisha kuwekeza Zanzibar na anawakaribisha pamoja na Kundi la Wafanyabiashara Wanawake kuitembelea Zanzibar.
Vilevile Mheshimiwa Rais Dk.Mwinyi alihojiwa na vituo viwili vikubwa vya China vinavyorusha matangazo kwa lugha ya Kiingereza.
Vituo hivyo ni China Global TV Network na baadae Shirika la Habari la China-XINHUA.
Mahojiano hayo yalijikita zaidi juu ya uhusiano wa China na Zanzibar na Tanzania kwa ujumla na sera za China barani Afrika.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi amerejea nchini leo tarehe 02 Julai 2023 baada ya kukamilisha ziara yake ya kikazi nchini China aliyoianza Jumanne tarehe 27June 2023.