Habari Tofauti

SEKTA BINAFSI NI MUHIMU KATIKA UWEKEZAJI WA BANDARI

Katibu Mkuu wa wizara ya Ujenzi na Uchukuzi anayesimamia Sekta ya Uchukuzi ,Gabriel Migire amesema pamoja na kazi kubwa inayofanywa Mamlaka ya usimamizi wa Bandari (TPA) ni muhimu kwa sekta binafsi kushirikishwa katika utoaji wa huduma katika Bandari ya Dar es Salaam ili kuongeza ufanisi.
Migire ameyasema hayo leo Julai Mosi,2023 jijini Dar es Salaam kwenye kikao cha Maboresho ya Bandari kilichowakutanisha wadau wa Bandari ikiwa pamoja na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari, Wizara ya Ujezi na Uchukuzi pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA.


“ Ili Bandari ifanye kazi kwa ufanisi ni muhimu kwa Sekta Binafsi kushirikiana na Serikali ili huduma katika Bandari zetu ziweze kuongeza ufaninisi , hivyo ni muhimu Sekta kuendelea kujitokeza na kuojiongezea uwezo wa kuongeza ufanisi wa kazi,” amesema Migire.
Kwa upande wake Ashraf Khan Mdau wa Bandari kwa zaidi ya Miaka 45 anasema Sekta Binafsi ni Muhimu kwa Kuongeza Ufanisi katika Bandari yoyote kwa kuwa kazi ya Bandari sio kupakua na kushusha tu Shehena na Mizigo .
“ Kazi ya Bandari ni kushusha, kupakia na kusafirisha kupeleka kwenye Bandari Kavu hii itasaidia sana kupunguza msongamano katika Bandari “ alisema Khan.
Naye Mwanasheria wa Wizara ya ujenzi na Uchukuzi Sekta ya Uchukuzi Mohamed Salum amesema katika makubaliano ya uwekezaji wa Bandari unazingatia wawekezaji wazawa hivyo kila Mwekezaji awe na uwezo kufanya kazi na waziwa.
Huku Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi- Sekta ya Uchukuzi Dokta Ally Possi ameasema kuwa mkataba haya nchini inafuta sheria za uwekazi ha Tanzania.

Back to top button