Habari Tofauti

WALIMU WA ELIMU YA AWALI WAFUNDWA

Angela Msimbira, KONDOA

JUMLA ya walimu wa awali 179 wamepewa mafunzo kuhusu mbinu za kuwafundisha watoto wa elimu ya awali ili kuwezesha ujifunzaji wa mtoto kulingana na hatua za makuzi.

Akitoa mada kuhusu mbinu bora za ufundishaji kwa watoto wa elimu ya awali mkufunzi, Julia Kaita Mpunga amesema kuwa ili mtoto aweze kuelewa mwalimu anapaswa kutumia mbinu mbalimbali za kufundisha zitakazomsaidia mtoto kujiamini na kuwa mahiri katika masomo.

Anazitaja mbinu za kumsaidia mtoto wa elimu ya awali kuelewa kwa haraka kuwa ni michezo ambayo humsaidia kutenda zaidi, kufikiri, kujiamini  na kunyoosha viungo.

Amesema mbinu nyingine ni hadidhi ambayo humsaidia kujua mambo mbalimbali ya zamani, kufurahisha, kufundisha na mbinu ya  nyimbo ambazo humfanya mtoto kufurahi, kucheza, kujifunza lugha na kuhesabu.

Naye Lianda Fransis  Mkufunzi kutoka Chuo cha Ualimu Butimba ambaye pia ni mwezeshaji wa mafunzo kwa walimu wa elimu ya awali katika Chuo cha ualimu Bustani Kondoa amesema kuinua ufaulu kwa watoto hususani kwa  ngazi ya elimu ya awali ambao ndio msingi katika kitovu cha elimu.

“Mtoto mdogo akielimushwa tunatarajia kuwa Taifa lililoelimika  ndio maana Serikali inasisitiza matumizi ya mbinu bora za ufundishaji  na jumuishi,” amesema Bi.Linda

Amesema mtumzi ya michezo humsaidia mtoto kukumbuka mafunzo aliyofundishwa darasani na humsaidia kukumbuka kile alichofundishwa  darasani hivyo kutamsidia kujenga umahiri kwa mtoto.

Back to top button