Kumbukumbu ya Uhuru wa Jamhuri ya Somalia
Somalia ilipata uhuru wake kamili mnamo 1960, wakati ambapo mwishoni mwa karne ya kumi na tisa,Waingereza na Waitalia walianzisha makoloni yao nchini Somalia, na sehemu iliyodhibitiwa na Uingereza ilijulikana kama Somalia ya Uingereza, na sehemu iliyotawaliwa na Italia ilijulikana kama Somalia ya Italia.
Mnamo Aprili 1960, Baraza la Sheria la Somalia ya Uingereza lilipitisha azimio la kuomba uhuru, na mabaraza ya sheria nchini yalikubali pendekezo hilo.
Somalia ya Italia iliungana na Somalia ya Uingereza na kuunda Jamuhuri ya Somalia, iliyopata uhuru mnamo Julai Mosi, 1960.
Misri na Somalia huunganishwa pamoja na mahusiano ya ndugu yenye kina yanayopanuka mnamo historia .na Misri ilikuwa moja ya nchi za kwanza kutambua uhuru wa Somalia mnamo 1960 na ilitoa misaada katika nyanja tofauti baada ya uhuru.