Habari

RAIS DK.MWINYI AMEZIKARIBISHA KAMPUNI ZAIDI ZA CHINA KUWEKEZA AFRIKA

0:00

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk .Hussein Ali amezikaribisha kampuni nyingi za China kuwekeza katika Bara la Afrika, kwani kuna ardhi ya kutosha, nguvu kazi nyingi na Afrika ina uthubutu wa kufanya biashara.

Dk. Mwinyi aliyasema hayo leo wakati wa sherehe za ufunguzi wa mkutano wa tatu wa ushirikiano wa Biashara kati ya China na Afrika, uliofanyika katika jiji la Changsha jimbo la Hunan China.

Dk. Mwinyi alisifu ushirikiano baina ya China na Tanzania ambao sasa umetimiza miaka 60 na akaonesha matumaini yake ushirikiano huo utazidi kukua na kuimarika.

Amesema katika miaka miwili iliyopia Afrika imeshuhudia ushirikiano mkubwa na China ambapo biashara imeongezeka kwa zaidi ya dola bilioni 74.

Amefurahi kuona wawekezaji wakubwa wa China wamehudhuria mkutano huo na akabainisha hiyo ni fursa kwa Afrika kujitutumua zaidi na kukaribisha wawekezaji hao barani humo.

Mapema akifungua mkutano huo kwa niaba ya Afrika Rais wa Malawi Lazaro Chikwera ametaka kuwe na mbinu madhubuti za kuzuia jaribio lolote la kupunguza kazi ya ushirikiano baina ya China na Afrika.

Amesema China na Afrika hazina tena muda wa kuzorotesha uhusiano huo na kuwataka Waafrika kutumia kwa vitendo yale yote waliyojifunza kwa muda wote wa ushirikiano na China.

DK.Chakwera amewataka Waafrika kutumia kipindi hiki kutangaza zaidi bidhaa zake mbalimbali.

Ameitaka China kufikiria kuanza kusamehe mikopo yake kwa Afrika hali itakayosaidia bara hilo kuendelea kupiga hatua za maendeleo.

Back to top button