Habari

RAIS DK.MWINYI AISHUKURU CHINA KWA MSAADA WA KITABIBU

Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi, ameishukuru serikali ya China kwa misaada ya kitabibu kwa Tanzania

Dk Mwinyi alieleza kwamba hadi sasa China imekwisha leta Tanzania matabibu zaidi ya 2000 kwa kipindi cha miongo sita ya uhusiano baina ya nchi mbili hizi.

Aliyaeleza hayo katika mkutano maalum wa sekta ya Afya kwa ushirikiano uliopo baina ya China na Tanzania, uliofanyika katika jiji la Changsha jimbo la Hunan.

Ameleza kufurahishwa na kazi kubwa inayofanywa na madaktari hao kutoka jimbo la Hunan.

Dk Mwinyi ametaka kuendelezwa zaidi ushirikiano baina ya watu wa sekta za Afya wa China na Tanzania, China waendelee kutoa misaada ya mafunzo ya kitabibu, pia aliwahimiza Wachina washajihishwe kuwekeza katika maduka ya dawa na kuwepo ushirikiano zaidi wa kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiiza.

Kesho ijumaa Rais wa Zanzibar anatarajiwa kukutana na makundi ya wafanyabishara na wawekezaji wa China.

Back to top button