Balozi wa Misri nchini Kenya ajadili kuimarisha biashara ya pande mbili na Waziri wa Uwekezaji, Biashara na Viwanda wa Kenya
Mervet Sakr
Balozi/ Wael Nasr El-Din Attiya, Balozi wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri nchini Kenya, alikutana na Bw. Moses Korea, Waziri wa Uwekezaji, Biashara na Viwanda wa Kenya, ambapo walijadili njia za kuimarisha biashara kati ya nchi hizo mbili, kunufaika na uanachama wao wa pamoja katika mkutano wa COMESA na kuamsha Makubaliano ya Biashara Huria ya Bara la Afrika yaliyozinduliwa mjini Sharm El-Sheikh mwaka wa 2015, tena njia mbadala za shughuli za kibiashara kwa sarafu za ndani.
Nasr El-Din aliangazia nia ya Misri ya kuendeleza mahusiano ya kibiashara na Kenya, mshirika wake mkubwa katika Afrika Mashariki na lango lake la masoko ya Afrika, akisisitiza kuwa ukombozi wa biashara kati ya nchi za bara hilo huunga mkono juhudi za ushirikiano wa kiuchumi na kutegemeana kati ya nchi za Afrika. Alieleza utayari wa Misri kukidhi mahitaji ya soko la Kenya la sukari na bidhaa nyingine za Misri, na nia yake ya kuongeza uagizaji wake kwa chai ya Kenya, akiita kuwezesha makampuni ya Misri kupata fursa za uwekezaji katika nyanja mbalimbali nchini Kenya, haswa Utalii na Ujenzi.
Waziri wa Kenya alisifu ushirikiano uliopo na Misri katika nyanja mbalimbali, akionesha kwamba kuna matarajio mapana ya kuimarishwa, haswa kuhusu kuongeza mabadilishano ya biashara na uwekezaji wa pande zote. Vile vile alielezea kukaribisha kwa nchi yake kwa makampuni ya Misri kuingia katika soko la Kenya na kutoa kile inachokihitaji, akisisitiza azma ya nchi yake kunufaika na utaalamu wa Misri katika nyanja za Nishati, Utalii, Shughuli za Hoteli na nyinginezo.