Habari

RAIS DK.MWINYI AKUTANA NA JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA WA UJERUMANI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Jumuiya ya wafanyabiashara wa Ujerumani leo tarehe 20 Juni 2023 Jijini Berlin.

Mkutano huo umejadili fursa za  uwekezaji na biashara zinazopatikana Zanzibar ikiwemo sekta ya uchumi wa buluu, maji safi na salama, umeme, elimu na  vyuo vya mafunzo ya amali, tehama, viwanda na usarifu wa mazao ya kilimo na sekta ya afya.

Aidha, Rais Dk.Mwinyi amewaahidi wafanyabiashara hao kuwa wote wanakaribishwa na Serikali ipo tayari kuwapokea na inawahakikishia usalama wa  uwekezaji na biashara zao.

Back to top button