Habari Tofauti

Wadau mbali mbali wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar washiriki katika ghafla ya kujadili na kutoa maoni yao juu sera za Tehama ya Chuo

Wadau mbali mbali kutoka Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar wameshiriki katika ghafla ya kujadili na kutoa maoni yao juu sera za Tehama ya Chuo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa HEET wa kuwajengea uwezo wafanyakazi wa chuo hicho.

Hafla hiyo inayofanyika kuanzia leo Mei, 27 hadi 28 katika kampasi ya Chuo cha Utalii Marubuhi kwa siku mbili ambapo lengo lake kuu ni kujadili na kutoa maoni katika sera hiyo kwa kujumuisha vipengele 14 ili kuboresha masuala ya teknolojia ya habari na mawasiliano.

Aidha, vipengele 14 vya muongozo katika sera vinajadiliwa ili kuboresha na kuongeza ufanisi katika Tehama, baadhi ya vipengele hivyo ni usimamizi wa Tehama, uongozi wa Tehama, matumizi ya miundo mbinu ya Tehama, matumizi ya mifumo ya mitandao, matumizi ya barua pepe, miongozo ya ufanyaji tafiti, kujifunza na ufundishaji, kuwajengea uwezo wafanyakazi, utunzaji wa taarifa pamoja na usambazaji wa taarifa za tehema chuoni.

Back to top button