Habari Tofauti

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha SUZA apongeza jumuiya ya Wajamama kwa kulisaidia taifa

0:00

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Prof. Moh’d Makame Haji ameipongeza jumuiya ya Wajamama kwa kulisaidia taifa hususani kina mama wajawazito.

Pongezi hizo amezitoa mara baada ya kuwekwa kwa saini katika mkataba wa makubaliano ya ushirikiano kati ya chuo  na jumuiya  yaliyofanyika kampasi ya Tunguu Zanzibar.

Prof. Makame amesema kuwa makubaliano hayo yatasaidia wanafunzi  wanaosoma sekta ya afya kwa ajili ya kufanya mafunzo yao kwa ufanisi na ufasaha zaidi. Makamu mkuu amefafanua kuwa makubaliano hayo yana lengo la kuimarisha mashirikiano sambasamba na kutatuwa changamoto za afya kwa taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake mkurugenzi wa jumuiya ya wajamama ngudu Nafisa Jiddawi amesema kwamba mkataba huo utakinufaisha chuo kikuu hicho  pamoja na taifa kwa ujumla, kwani wamejipanga kuwaleta wataalamu wa afya kutoka nje ya  nchi mbali mbali ikiwemo Marekani  ili kuweza kuja kuwafunza zaidi walimu na wanafunzi wa chuo hicho.

Back to top button