Habari Tofauti
Makamu wa Rais wa Tanzania afanya mazungumzo na Rais Mteule wa Mkutano wa Cop 28

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akifanya mazungumzo na Rais Mteule wa Mkutano wa Kimataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (Cop 28) Dkt. Sultan bin Ahmed Al Jaber ambaye pia ni mjumbe maalum wa Serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) katika masuala ya mabadiliko ya tabianchi. Mazungumzo hayo yamefanyika katika kituo cha mikutano cha Sharm El Sheikh nchini Misri leo tarehe 23 Mei 2023.












