Habari Tofauti

HAKUNA KIFO CHOCHOTE KILICHOTHIBITISHA KUWA NI UVIKO

NA WAF- DODOMA

WAZIRI wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amewatoa hofu wananchi kwa kuweka wazi kuwa, mpaka sasa hakuna kifo chochote kilichothibitisha kusababishwa na ugonjwa wa UVIKO na kuwataka wananchi kuwa watulivu wakati Serikali ikiendelea kufuatilia hali hiyo.

Waziri Ummy amesema hayo,  kupitia mtandao wake wa kijamii, kufuatia hali ya sintofahamu inayoendelea kupitia mitandao ya kijamii mbalimbali juu ya kuibuka kwa ugonjwa wa UVIKO nchini na kusababisha vifo.

Ametoa rai kwa  wananchi kuondoa hofu wakati Serikali ikiendelea kuchakata taarifa ilizokusanya kutoka kwenye vituo vya kutolea huduma mbalimbali ndani ya wiki, na kuahidi kutoa taarifa ili kuujuza umma juu ya hali hiyo.

Ameendelea kusema, Kwa taarifa za wagonjwa waliopimwa virusi vya UVIKO wiki ya tarehe 6 – 12 Mei 2023 Watu 6 kati ya 288 walithibitishwa kuwa na ugonjwa huo, ikiwa ni pungufu ikilinganishwa na wiki ya tarehe 29/04/23 hadi 05/05/23.

Aidha, Waziri Ummy amewatoa hofu wananchi kwa kuweka wazi kuwa, mpaka sasa Hakuna kifo chochote kilicho thibitishwa kusababishwa kutokana na ugonjwa wa UVIKO-19,

Sambamba na hilo, amewataka wananchi kuzingatia kanuni za afya na  usafi.

Back to top button