Katibu Mkuu wa Shirika la Ushirikiano wa Maendeleo la Misri akutana na baadhi ya wanafunzi kutoka nchi ndugu za Afrika wanaosoma nchini Misri
Mervet Sakr

Ndani ya mfumo wa kufuatilia hali ya wanafunzi waafrika wanaosoma katika Kitivo cha Tiba, Chuo Kikuu cha Ain Shams na wapokeaji wa misaada iliyotolewa na Shirika la Ushirikiano wa Misri kwa Maendeleo, Balozi Ashraf Ibrahim, Katibu Mkuu wa Shirika la Ushirikiano la Misri, alikutana na wanafunzi 25 kutoka nchi za Afrika. Wakati wa mkutano huo, Katibu Mkuu alisisitiza umuhimu wa Serikali ya Misri kushikamana na kusaidia nchi za Afrika kupitia shughuli za Shirika, akifafanua kuwa udhamini unaotolewa na Shirika ni moja ya shughuli za Shirika na lengo la kuhamisha uzoefu katika nyanja ambazo usomi hutolewa.
Aidha, Katibu Mkuu ameongeza kuwa misaada inayotolewa katika fani ya utafiti wa tiba inalenga kusaidia uwezo wa huduma za afya katika nchi za kindugu za Afrika ili kufikia malengo ya maendeleo endelevu. Wanafunzi hao pia wameelezea furaha yao kubwa kwa kupata fursa ya kusoma nchini Misri kupitia Shirika la Ushirikiano la Misri.
Mkutano huo ulishughulikia majadiliano kati ya wanafunzi na Katibu Mkuu kuhusu wasiwasi na changamoto zinazowakabili wanafunzi katika masomo hayo, ambapo Katibu Mkuu alisisitiza kuendelea kwa juhudi za hali ya juu ili kuondokana na vikwazo vyovyote vinavyoweza kutokea kwa wanafunzi wakati wa masomo yao nchini Misri. Pia alisisitiza nia ya serikali ya Misri kusaidia hali ya elimu na afya katika bara la Afrika ili kufikia Malengo ya Maendeleo ya Umoja wa Mataifa 2030.










