Habari Tofauti

Kozi za mafunzo katika Kitivo cha Mafunzo ya Juu ya Afrika, Chuo Kikuu cha Kairo; kufundisha lugha kuu za kiafrika na maarufu zaidi

Mervet Sakr

0:00

Kituo cha Kufundisha Lugha za Kiafrika katika Kitivo cha Mafunzo ya Juu ya Afrika, Chuo Kikuu cha Kairo, pamoja na Uangalifu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kairo, Mohamed Osman Elkhosht na Mkuu wa Kitivo Attia El-Tantawy, huandaa kozi kadhaa za mafunzo ya kufundisha lugha kuu za Kiafrika zinazoenea zaidi Barani Afrika, ambazo ni: (Kiswahili – Kihausa – Kiamhari – Kifulani – Kisomali) kwa lengo la kufungua madaraja ya mawasiliano na maelewano kati ya Misri na nchi za Afrika kwa wazungumzaji wa lugha hizo, kufungua hadi Afrika na kuimarisha mawasiliano na ushirikiano na nchi na watu.

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kairo, Dkt. Mohamed Osman Elkhosht amesema kuwa Chuo Kikuu cha Kairo kinazingatia faili la Afrika, kinaunga mkono jukumu kubwa la Misri Barani Afrika, kinaongeza kutegemeana na kuridhiana na nchi nyingine za Afrika, na kinaunga mkono mahusiano ya kihistoria na maslahi muhimu kati ya Misri na mazingira yake ya Kiafrika ili kufikia ushirikiano wa Afrika kwa maana yake pana,akisisitiza kuwa Kitivo cha Mafunzo ya juu ha Kiafrika ya katika Chuo Kikuu hicho ni Jukwaa kubwa sana katika taaluma zote na masuala ya Afrika, na hutumia utaalamu wake na uwezo wa utafiti na huduma kama nyumba ya utaalamu Barani Afrika, pamoja na jukumu la kitivo katika kuimarisha ujuzi wa mambo ya bara la Afrika, na kusukuma na kuimarisha mahusiano ya Kimisri na Kiarabu pamoja na Afrika.

Kwa upande wake, Dkt. Attia El-Tantawy, Mkuu wa Kitivo cha Mafunzo ya Juu ya Kiafrika, alisema kuwa Kituo cha Kufundisha Lugha za Kiafrika kilianzishwa mwaka 2019, sambamba na urais wa Misri wa Umoja wa Afrika, ili kiwe kituo cha kwanza kuanzishwa katika vyuo vikuu vya Misri na Kiarabu kwa lengo la kufundisha lugha za Kiafrika na kuwa na jukumu muhimu katika kuhudumia mwenendo na maslahi ya Misri Barani Afrika, akieleza kuwa kituo hicho kinalenga kutoa kozi za mafunzo na huduma za Ufasiri kutoka na kuelekea lugha za Kiafrika ili kuandaa mfasiri au mwalimu wa lugha ya Kiafrika kwa kiasi kikubwa kutoka ujuzi na ufanisi, pamoja na jukumu lililotekelezwa na kituo katika kueneza utamaduni wazi kwa bara na kuimarisha mawasiliano miongoni mwa watu wake.

Back to top button