Balozi wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri mjini Kampala akutana na Waziri wa Biashara, Viwanda na Ushirika wa Uganda
Mervet Sakr

Balozi Munther Selim, Balozi wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri mjini Kampala, Mshauri wa Kibiashara Ahmed Seif El-Nasr na Mwanadiplomasia Attaché Mohamed Abdo wamekutana na Bw. Francis Mwebesa, Waziri wa Biashara, Viwanda na Ushirika wa Uganda ambapo walipitia masuala kadhaa yenye maslahi ya pamoja, pamoja na kuimarisha mahusiano kati ya Misri na Uganda katika nyanja za biashara na uwekezaji.
Wakati wa mkutano huo, Balozi huyo wa Misri aliangazia kiwango kikubwa cha mabadilishano ya kibiashara kati ya nchi hizo mbili mnamo miaka iliyopita, na maslahi ya Jumuiya ya viwanda ya Misri katika kipindi cha sasa kuwapo katika soko la Uganda kibiashara na uwekezaji pia uliguswa kupitia ziara nyingi za wafanyabiashara wa Misri kukutana na wenzao pembezoni mwa maonesho na vikao vya biashara vilivyoandaliwa nchini humo ndani ya muktadha wa fursa kubwa zinazopatikana kwa wafanyabiashara kutoka pande zote mbili.
Walizungumzia jukumu la uongozi la Misri kama moja ya nchi wanachama wakubwa wenye muundo mashuhuri wa viwanda na usafirishaji katika makubaliano ya COMESA, na kusisitiza umuhimu wa kujitolea kwa upande wa Uganda kwa punguzo la forodha linalopaswa kutolewa kwa kampuni za Misri ndani ya muktadha wa makubaliano ya COMESA, kwa sababu ya athari zake chanya katika kusukuma mahusiano ya kibiashara mbele na kuongeza upatikanaji wa mauzo ya nje ya Misri ya bidhaa mbalimbali kwenye soko la Uganda, haswa kwa maendeleo makubwa sekta ya viwanda nchini Misri inayoshuhudia kwa sasa, pamoja na umuhimu wa kuendeleza mifumo ya ushirikiano wa ziada kwa lengo la Utekelezaji wa miradi ya ziada katika kipindi kijacho unaolenga kugundua fursa zaidi za ushirikiano kati ya pande hizo mbili.