Habari Tofauti

MAMA MARIAM MWINYI ATOA SADAKA KATIKA VITUO VYA KULEA WAZEE NA WATOTO ZANZIBAR

Ahmed Hassan

 

 

Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) amesema Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni mwezi wa kuwasaidia watoto yatima, wajane ,walemavu na wazee wasiojiweza wenye mahitaji maalum ili kupata futari .

Mama Mariam Mwinyi ameyaeleza hayo leo, pia alipotembeleavituo vya kulea wazee na watoto Welezo, Sebleni, SOS na kituo cha nyumba ya watoto Mazizini na kutoa sadaka ya vyakula pamoja na mabegi ya shule kwa wanafunzi.

Aidha, Mama Mariam ametoa wito kwa watu wenye uwezo kuzidisha zaidi kusaidia wasiojiweza katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani .

Back to top button