SERIKALI IPO LETENI CHANGAMOTO ZENU WAFANYABIASHARA TUTAWASAIDIA KUZITATUA
Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Taifa la Zanzibar (ZNBC) , Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amezitaka Wizara na wadau wa sekta mbalimbali zinazofanya biashara wakutane kila Miezi mitatu kujadiliana kuhusu changamoto na kuzipatia ufumbuzi. Pia amelitaka Baraza la biashara la Taifa kukutana kila baada ya Miezi sita huku Jukwaa likutane mara moja kwa Mwaka katika kuongeza ufanisi zaidi kwa utatuzi wa changamoto za biashara nchini.
Aliyasema hayo wakati alipofungua Jukwaa la Kumi na Mbili la biashara leo tarehe 19 Machi , 2023 lilifanyika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Airport.
Aidha , Dk.Mwinyi amegusia maazimio ya Baraza hilo ikiwemo masuala ya kodi na kuwataka Wizara ya Fedha ,TRA na ZRA wakutane na kujadiliana hili kuyatatua huku wakipeleka taarifa za utatuzi wa changamoto hizo katika jukwaa .
Vilevile, alieleza kuwa Serikali ipo kutatua changamoto kwa ufumbuzi zaidi na Wafanyabiashara wapeleke changamoto zao watasaidiwa.