Balozi wa Misri nchini Sudan Kusini akutana na Mwenyekiti wa tume ya pamoja ya Ufuatiliaji na Tathmini
Mervet Sakr
Balozi Moataz Mostafa Abdel Qader, Balozi wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri mjini Juba, amempokea Mwenyekiti wa Tume ya Pamoja ya Ufuatiliaji na Tathmini, Luteni Jenerali Charles Gateway, na kikundi chake cha kazi, ambapo mkutano huo uligusia mchango mkubwa wa Tume katika kufuatilia utekelezaji wa matakwa ya makubaliano ya Amani yaliyofufuliwa nchini Sudan Kusini.
Katika mkutano huo, Luteni Jenerali Gateway alipitia majukumu na michango ya Tume na mamlaka yake ya kufuatilia na kushughulikia hali ya utekelezaji wa matakwa ya makubaliano ya amani, pamoja na kuzishauri pande husika namna ya kusonga mbele katika kutekeleza masharti ya makubaliano hayo, ambayo Balozi Abdul Qader aliyapongeza, akisifu juhudi zao tajiri na muhimu katika kufuatilia utekelezaji wa mapatano ya mikataba, pamoja na kuwasilisha mapendekezo kwa pande husika juu ya namna ya kusonga mbele. Pande hizo mbili pia zilijadili maendeleo ya ndani ya nchi ya hivi karibuni na jitihada mbalimbali za kuyadhibiti.
Katika muktadha unaohusiana, pande hizo mbili zilijadili matarajio ya ushirikiano wa baadaye kati ya Jamhuri ya Kiarabu ya Misri na Tume ya Pamoja ya Ufuatiliaji na Tathmini, kwa kuzingatia mahusiano yaliyotukuka na jukumu maarufu la Misri nchini Sudan Kusini.