HabariUchumi

RAIS DK.MWINYI AMESEMA ZANZIBAR IPO TAYARI KUIONYESHA DUNIA FURSA KUPITIA KILIMO CHA MWANI NA UVUVI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar ipo tayari kuionyesha Dunia fursa zinazopatikana kupitia kilimo cha mwani na uvuvi .Aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika AGRF, 2023 uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan Ikulu ,Dar es Salaam.

Dk.Mwinyi amempongeza Rais Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa mafanikio chini ya Uongozi wake na jitihada zake zimeiwezesha Tanzania kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Mkutano huo kwa dhamira yake ya kumkomboa mwananchi kwa kutengeneza fursa za ajira miongoni mwa Vijana na Wanawake katika sekta ya Kilimo.

 

Aidha , Dk.Mwinyi amesema nchi yetu ina fursa kubwa ya Uwekezaji katika sekta ya kilimo kwa hivyo kupitia mkutano huo itatoa fursa ya ufafanuzi kwa kina na kuvutia uwekezaji kwa Dunia kufahamu fursa zinazopatikana Tanzania katika kilimo.

Vilevile, Dk.Mwinyi alieleza Mkutano huo utafungua fursa nyingi za ajira kupitia kilimo cha mkataba , fursa za masoko ya bidhaa zitakazozalishwa kupitia ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imeahidi kutoa ajira milioni 3 kwa Tanzania Bara na laki 3 kwa Zanzibar .

Back to top button