Waziri wa Vijana na Michezo akutana na mwenzake nchini Nigeria kujadili njia za ushirikiano wa pamoja kati ya pande hizo mbili
Mervet Sakr

Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alikutana na Sunday Dari, Waziri wa Vijana na Maendeleo ya Michezo wa Nigeria; kujadili njia za ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, mbele ya Balozi wa Jimbo la Nigeria nchini Misri, Dkt. Adel Radwan, Mkuu wa Sekta ya Michezo, na Meja Jenerali Ismail Al-Far, Mkuu wa Sekta ya Vijana.
Mkutano huo ulishughulikia uratibu katika sekta ya michezo nchini Nigeria, na mchakato wa kuunganisha sekta binafsi na mashirika ya kiraia katika maendeleo ya huduma za michezo na maendeleo ya miundombinu nchini Nigeria.
Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alimkaribisha mwenzake wa Nigeria nchini Misri, akisisitiza kina cha mahusiano ya zamani kati ya nchi hizo mbili ndugu, akibainisha kuwa kipindi kijacho kitashuhudia maendeleo makubwa katika ushirikiano kati ya pande hizo mbili katika nyanja za Vijana na Michezo.
Wakati Waziri wa Vijana na Michezo akieleza kuwa sekta ya michezo Duniani kote imekuwa lazima na sayansi, kwani nchi nyingi Duniani zinapata mafanikio mengi kutokana na sekta ya michezo, hivyo taifa la Misri linajitahidi kuongeza sekta ya michezo nchini Misri na kupata faida kubwa inayoweza kunufaika katika mambo mengi kwa jamii ya Misri, ikiwa ni pamoja na kupunguza ukosefu wa ajira na viwango vya juu vya mapato ya kila mtu, na kutoa sarafu ngumu, inayopunguza mzigo kwa serikali na kusaidia maendeleo katika mengi ya maeneo mengine.
Kwa upande wake, Sunday Dari, Waziri wa Vijana na Maendeleo ya Michezo nchini Nigeria, alielezea kufurahishwa kwake na mkutano wa kimataifa wa michezo na maonesho “Maonesho ya Michezo”, ambayo yalitekelezwa na Wizara ya Vijana na Michezo ya Misri, akibainisha kuwa anataka uratibu wa pamoja kati ya wizara hizo mbili ili kusaidia kuandaa mkutano wa kimataifa na maonyesho sawa na yale yaliyoandaliwa na Misri, lakini nchini Nigeria.
Alibainisha kuwa Nigeria ina idadi kubwa ya vijana, kwani 75 % ya idadi yote ya watu ni chini ya umri wa miaka 25, hivyo Wizara ya Vijana na Maendeleo ya Michezo inataka kutoa huduma bora na kunufaika na utaalamu wote unaowezekana ili kuitoa kwa jamii ya Nigeria.
Alimalizia akisema: “Tunatamani kutumia utaalamu wa Misri katika kuandaa mkutano wa kimataifa na maonyesho, ili kutekeleza mkutano nchini Nigeria, akisema kuwa taifa la Misri lina uzoefu mwingi tunaotafuta ushirikiano kati yetu.”
Alihitimisha hotuba yake akisisitiza kuwa taifa la Misri limeshuhudia kushamiri kwa miundombinu na huduma za vijana na michezo zilizokuwa zikitekelezwa, kwani anatarajiwa kuzuru mji mkuu mpya wa utawala na mji wa Olimpiki wa Misri.
Pande hizo mbili zilikubaliana kuwa mnamo kipindi kijacho, mkataba wa maelewano utasainiwa kati ya pande hizo mbili katika nyanja za Vijana na Michezo na kubadilishana uzoefu kati ya pande hizo mbili.