Balozi wa Misri nchini Azerbaijan atoa taarifa ya Misri kwa Mkutano wa Kilele wa Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote wa Kikundi cha Mawasiliano ya Kukabiliana na COVID-19
Mervet Sakr

Balozi Hisham Nagy wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri mjini Baku kwa niaba ya Rais Abdel Fattah El-Sisi, mnamo Machi 2, 2023,aliitoa taarifa ya Misri kabla ya mkutano wa Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote katika ngazi ya mkutano wa kundi la mawasiliano kuhusu kukabiliana na COVID-19.
Mwanzoni mwa hotuba yake, Balozi wa Misri aliwasilisha kwa hadhira salamu za Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, ambaye majukumu yake mingi yalimzuia kushiriki katika mkutano huo, na pia alimshukuru Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev kwa mpango wake wa kufanya mkutano huu muhimu, akisifu uenyekiti hai wa Azerbaijan wa Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote.
Taarifa ya Misri ilisisitiza umuhimu wa Misri kushikamana na harakati ya kutofungamana kwa upande wowote katika wakati huu wa kihistoria katika uwanja wa kimataifa, unaoshuhudia kurejea kwa migogoro kwa upande mmoja, na ambapo ulimwengu unakabiliwa na changamoto kadhaa zimezoathiri nyanja zote za maisha, kama vile mabadiliko ya hali ya hewa, mgogoro wa chakula na majanga ya kimataifa kwa upande mwingine, inayohitaji kuimarisha ushirikiano wa nchi za Harakati na kufanya kazi ili kuziamsha kuongoza harakati za kimataifa kushughulikia masuala muhimu kwa manufaa ya binadamu.
Kwa muktadha huo, Balozi wa Misri alipitisha hatua zilizochukuliwa na Misri ili kudhibiti athari nyingi za janga la Corona kupitia sera za kifedha, kiuchumi na kijamii zimezoonesha mafanikio na ufanisi, zilizoiwezesha kufikia viwango chanya vya ukuaji na kupunguza viwango vya ukosefu wa ajira dhidi ya matatizo yote, zilizochangia kujenga hali ya utulivu na imani ya kimataifa juu ya uwezo wa uchumi wa Misri kuhimili na kunyonya na kuondokana na migogoro.
Balozi Hisham Nagy pia alieleza kuwa licha ya mgogoro huo, Misri pia iliweza kutekeleza mipango kabambe ya kuinua kiwango cha maisha ya raia katika maeneo yenye uhitaji mkubwa kupitia mpango wa “Maisha bora”, na kupanua wavu wa usalama wa kijamii kwa mamia ya maelfu ya familia kupitia mpango wa “Takaful na Karama”, uliochangia kupunguza mzigo wa janga hilo, pamoja na juhudi za Misri za kukuza ujumuishaji wa kifedha, kuunganisha uchumi sambamba na digitalization, pamoja na kuandaa mkakati wa kitaifa wa haki za binadamu unaojumuisha haki ya kufanya kazi.