Habari Tofauti

MAMA ZAINAB: TAASISI ZA KUSAIDIA YATIMA ZITUMIKE KUINUFAISHA JAMII

Ahmed Hassan

0:00

Mwenyekiti wa Taasisi ya Nuru Foundation Zanzibar Mama Zainab Kombo Shaib, amesema ipo haja ya kuzitumia vyema taasisi za kusaidia watoto yatima ili kuisaidia Serikali na Jamii kwa ujumla.
Mama Zainab ambaye pia ni Mke wa Makamu wa Kwanza Wa Rais wa Zanzibar, ameyasema hayo leo Machi 05, wakati wa utambulisho wa Ofisi ya Nuru Foundation, Tawi la Pemba uliofanyika Gombani Mkoa wa Kusini Pemba.
Amesema misaada inayotolewa kwaajili ya watoto, watu wenye ulemavu, wazee wasiojiweza na makundi maalum ikiwafikia ipaswavyo, itasaidia katika kujikwamua kimaisha hususan katika kipindi hichi cha kuelekea Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Bi. Zainab amesema pamoja na harakati nyenginezo zinazolenga kusaidia jamii, Taasisi yake kwasasa inajikita zaidi katika kuboresha afya ya mama na mtoto kwa kuanza kuwapatia bima za afya watoto yatima na wenye mazingira magumu.
Aidha amesema taasisi yao inao mpango wa kutatua changamoto ya saratani ya shingo ya kizazi kwa akinamama.
“Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 6.7 kwa Kisiwa cha Pemba, na 1.6 kwa Unguja, wanakabiliwa na changamoto ya saratani hii, tunajipanga kutoa elimu sambamba na kuleta wataalamu ili kupambana na tatizo hili” amesema Mama Zainab akisisitiza kuanzia kampeni hio katika maskuli ili kutoa elimu kwa mabinti.
Mama Zainab ametoa wito kwa taasisi zinazojihusisha na kukusanya misaada kwalengo la kuwapatia watoto yatima, kuwalenga kwa udhati wahitaji, na siyo kutumia mwevuli huo kwa maslahi binafsi.
Naye Mratibu wa ‘NGO’ kwa upande wa Kisiwa cha Pemba Bw. Ashrak Hamad, amesema jitihada zaidi zinahitajika ili kuwanusuru watoto yatima na wenye mazingira magumu na kuwaepusha kujiingiza katika mabalaa likiwemo wimbi la madawa ya kulevya.
Akitoa salamu kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mkuu wa Wilaya ya Mkoani, Bw. Khatib Juma Mjaja, amesema taasisi zenye mnasaba wa kusaidia ikiwemo Nuru Foundation, zinao wajibu wa kuongeza nguvu zaidi katika jamii, hasa kisiwani Pemba kwani mahitaji yanazidi kuwa makubwa, siku hadi siku.
” Nuru Foundation mumekuwa wadau wakubwa wa kusaidia mayatima, watoto wenye ulemavu na wenye mazingira magumu, ila tunawaomba
Back to top button