
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa . Aweso (Mb) ameielekeza Mamlaka ya Majisafi Arusha AUWSA kufanyia kazi na kutatua kwa wakati kero za wananchi.
Maelekezo hayo ameyatoa katika kikao kazi alichokifanya na Bodi ya Wakurugenzi pamoja na Menejimenti ya AUWSA jijinii Arusha.
“Watendaji wasizoee shida za wananchi, Kero na matatizo yote kama vile maunganisho mapya, mivujo, ankara, na huduma kwa wateja yasikilizwe na kushughulikiwe kwa wakati.” Waziri Aweso kasema.
Aidha, ameitaka AUWSA kuhakikisha wananchi wa Jiji la Arusha wanapata huduma ya Maji iliyoimarika na inayoridhisha na kwenye changamoto, AUWSA ishirikiane na viongozi wa jamii husika katika kupata suluhisho kwa manufaa ya Watanzania kwa Ujumla.
Kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi AUWSA, Balozi Mhe. Daniel Ole Njoolay alimshukuru Mhe. Waziri Aweso kwa kutenga muda wake na kuongea na Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya AUWSA kwa lengo la kuboresha huduma inayotolewa na Mamlaka kwa Wananchi wa Jiji la Arusha.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa AUWSA Mhandisi Justine Rujomba, ameeleza kuwa Menejimenti na watumishi wote wa wamepokea maelekezo yote na ushauri uliotolewa katika kikao hicho, hususan kwa AUWSA kuendelea kujiimarisha kwenye masuala ya uadilifu, uaminifu, na uhusiano kwa wateja .