Waziri wa Michezo asifu mafanikio ya ujumbe wa Misri katika Michuano ya mazoezi ya viungo ya Afrika nchini Morocco, na ubora wa ujumbe wa Karate katika Ligi ya Dunia huko Emirates
Ali Mahmoud

Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alisifu matokeo ya ujumbe wa Timu ya kitaifa ya mazoezi ya viungo katika Mashindano ya Afrika “Trampoline”, yaliyofanyika Morocco, pamoja na matokeo ya ujumbe wa Timu ya Karate unaoshiriki katika Michuano ya Ligi ya Dunia kwa vijana wachipukizi na vijana huko Fujairah, UAE.
Ujumbe wa Misri uliweza kufikia medali 4 katika Michuano ya Afrika ya mazoezi ya viungo, nazo ni medali ya dhahabu kwa mchezaji Ashrakat Ismail, na medali ya fedha kwa mchezaji Maryam El-Bayly katika mashindano ya wanawake, na kushinda medali ya dhahabu kwa Timu ya Wanaume wa Misri inayojumuisha wachezaji “Mohab Hassan, Safi El-Din Ismail, Nour El-Bahat, Khaled Hussein”, na katika mashindano ya mtu mmoja mmoja kwa wanaume, mchezaji Mohab Hassan alipata medali ya fedha.
Katika Mashindano ya Ligi ya Dunia huko Fujairah, ujumbe wa Misri ulishinda medali 17 anuwai ambazo ni medali 5 za dhahabu, medali 5 za fedha, na medali 7 za shaba.
Waziri wa Michezo aliwapongeza wachezaji wa timu za kitaifa wa kiume na wa kike kwa matokeo bora waliyopata kwenye Mashindano ya mazoezi ya viungo ya Afrika na Ligi ya Karate ya Dunia, kurekodi mafanikio mapya kwa mchezo wa Misri, ambao kwa sasa unashuhudia mafanikio mengi na ubora katika michezo ya mtu binafsi katika mikusanyiko mbalimbali ya kimataifa.
Walioshinda medali za dhahabu katika Ligi ya Karate ya Dunia ni: “Menna Allah Al-Hawary, Farah Salama, Youssef Ibrahim, Sajid Shahin, Salah Shawky”, wakati ambapo waliopata medali za fedha ni: “Abdul Rahman Tolba, Baher Abdo Nassif, Shahd Abdul Rahman, Malak Fahmy, Malak Qaoud”.
Walioshinda medali za shaba katika Ligi ya Karate ya Dunia ni: “Adam Tahseen, Gena Raafat, Muhammed Hani, Yassin Hassan, Fatima Muhammed Diasti, Jana Muhammed Shataifa, Habiba Khalil”.